Thursday, July 10, 2014

Wesley Sneijder anaweza kuwa huru kujiunga na Manchester United ikiwa Dau la Pauni Milioni 15.9 litatolewa ambacho ndio Kiwango kilichopo kwenye Mkataba wa Mchezaji huyo wa Netherlands kuruhusiwa kuihama Galatasaray ndani ya muda wa Mkataba wake. 
Inasadikiwa Man United, baada kumchukua Meneja mpya Louis van Gaal ambae sasa yuko pamoja na Sneijder huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia wakiwa na Netherlands, inataka kumsaini Kiungo huyo wa Miaka 30 kufuatia mapendekezo ya Van Gaal.
Mwezi uliopita, huko Brazil, Sneijder alifichua kuwa itakuwa ngumu kwake kuikataa nafasi ya kucheza chini ya Van Gaal.
Akiongea kwenye Mahojiano na Wanahabari wakati wa kumtambulisha Meneja wao mpya Cesare Prandelli, Rais wa Galatasaray, Unal Aysal, amesema: “Sneijder ni Mchezaji mzuri. Tunataka abaki Galatasaray lakini tukipata Euro Milioni 20 hatuwezi kumzuia. Hilo lipo kwenye Mkataba wake.”
Man United tayari imeshatumia Pauni Milioni 60 kuwanunua Wachezaji wapyya wawili Ander Herrera na Luke Shaw huku Thomas Vermaelen wa Arsenal akitajwa kuwafuata hao na Juventus kuitaka Man United kulipa Pauni Milioni 45 ikiwa wanamtaka Kiungo wa Chile Arturo Vidal.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog