Wednesday, July 9, 2014

Wafungaji mabao ya Ujerumani
Ujerumandiyo timu ya kwanza kufuzu kwenye Fainali ya kombe la dunia Brazil 2014, baada ya kuinyeshea wenyeji Brazil mabao 7-1 katika uwanja wa Estadio Mineirao ulioko Belo Horizonte.
Umakini wa vijana wa Joachim Low ulikuwa wa kupigiwa mfano walipoiadhibu Brazil na kuwa timu ya kwanza kuwahi kushindwa kwa mabao mengi zaidi katika hatua hiyo ya nusu fainali ya kombe la dunia.
Kabla ya mechi hiyo vyombo vya habari vilikuwa vimemulika mfumo wake Luiz Felipe Scolari vikidai alikuwa ameumba timu yake kumtegemea Neymar.
Kujeruhiwa kwa Neymar Ijumaa iliyopita ilimlazimu Scolari kubadili mfumo ambao sasa haukuwa na nyota huyo.
Je Scolari atasingizia nini ?
Fernandinho akiuhuzunika baada ya kutingwa bao la 5 na Ujerumani
Ilikuwa wazi tofauti ya mbinu za makocha hao wawili wajerumani walipoanza kwa kuwashirikisha washambulizi Miroslav Klose,Thomas Muller na Mesut Ozil huku Schweinsteigerakiwaongoza Toni Krooos Khedira na Lahm katika kiungo cha Kati.
Na Baada ya nipe nikupe ya kufungua mechi Iliwachukuwa Wajerumani takriban dakika kumi tu za kwanza kupenya safu ya ulinzi ya Brazil iliyokuwa inakosa uzoefu wa Thiago Silva.
Kilio kimetanda Brazil.
Thomas Muller alifungua kivuno hicho cha mabao kabla ya Klose kuidhibitishia Ujerumani fainali yao kombe la dunia kwa mkwaju uliomwacha kipa wa Brazil Julio Cesar asijue la Kufanya.
Klose kwa ushirikiano na Toni Kroos walifunga bao la tatu na la nne katika kipindi cha dakika moja.
Sami Kheidira alifunga la tano kunako dakika ya 29 kabla ya mchezaji wa akiba Andre Schurrle kufunga mabao ya 6 na ya 7 .
Bao la kufutia machozi la Brazil lilifungwa na Oscar kunako dakika ya mwisho ya mechi hiyo.
00:90 Oscar anaiifungia Brazil bao la kufutia machozi katika dakika ya mwisho ya mechi hii ya kihistoria .
00:70 Andre Schurrleanafanya mambo kuwa 6-0 kwa Ujerumani.
00:70 GOOOOOOOAL
Julio Cesar haamini dunia imempasukia wapi .
00:60 Ujerumani 5- Brazil
00:59 Miroslav Klose anapumzishwa Andre Schurrle anaingia
Bao la Milaslav Klose
00:58 Brazil inaendelea kutafuta angalau bao la kufutia machozi lakini Nuer hapishi
00:57
00:54' Kipa Manuel Nuer anainyima brazil bao la kufutia machozi
23:35
23:30 Ujerumani 5-0 Brazil
23:26
Ujerumani 1-0 Brazil
23:26 Toni KROOOOOS
23:24 GOOOOOOAL !Toni KROOOOS
23:20 Thomas Muller anafunga bao la pili la Ujerumani
23:20 GOOOOOOAL
23:20 Ujerumani 2-0 Brazil
Bao la Muller
Ujerumani hawajawahi kushindwa katika mechi ambayo wametangulia kufunga.
23:18 Brazil wanaonekana wameduwazwa na bao hilo la Muller
23:15 Kona kuelekea upande wa Ujerumani
23:11 Ujerumani 1-0 Brazil
23:10 Thomas Muller anaiweka Ujerumani mbele 1-0
23:10 GOOOOOOOOOAL
Muller akishangilia bao lake
23:10 Kona kuelekea lango la Brazil.
23:09 David Luiz analazimika kufanya kazi ya ziada kufuatia mashambulizi ya mjerumani
23:05 Ujerumani inashambulia lango la Brazil lakini wapi inazimwa .
23:02 Ujerumani 0-0 Brazil
23:01 Ujerumani haina matatizo ya wachezaji ikilinganishwa na Scolari ambaye amelazimika kuchezesha kikosi bila ya Neymar
Timu ya Ujerumani
23:00 Mechi Imeanza
Timu ya taifa ya Brazil itakavyokuwa katika mechi hii bila ya Neymar
22:57
22:55 Wimbo wa taifa wa Brazil unapigwa hapa uwanjani ,,mashabiki wa Brazil wanaimba
22:54 Wimbo wa taifa wqa Ujerumani unachezwa hapa mbele ya uwanja uliofurika furifuri
22:52Mashabiki wa Brazil na wale wa Ujerumani wakishangilia timu zao kabla ya mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia .
Brazil inachuana Ujerumani
22:50
22:50Wenyeji wa kombe la dunia Brazil wanachuana na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog