Wednesday, July 9, 2014


KAMPUNI kubwa ya vifaa vya michezo ya Nike ya Marekani inatarajiwa kutoongeza mkataba mwingine wa kuitengenezea jezi timu ya Manchester United kutokana na gharama za mkataba mpya. Nike wamekuwa wakitengeneza jezi maarufu za United toka mwaka 2002 na mkataba wao unatarajiwa kumalizika mwakani. Kuondoka kwa Nike kunatarajiwa kutengeneza njia kwa kampuni nyingine ya vifaa vya michezo ya Ujerumani Adidas kuingia mkataba mpya na klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford. United imetengeneza kiasi cha paundi milioni 38 katika mkataba walioingia na Nike kwa mwaka 2012-2013, yakiwemo magwanyo ya faida kutokana na mauzo ya bidhaa zake zenye nembo hiyo duniani. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa United sasa wanataka mkataba mpya ambao utakuwa thamani ya paundi milioni 60, kiasi ambacho Nike hawako tayari kukilipa.Jezi mpya ya Man United kwa ajili ya msimu mpya 2014/15 Nyumbani

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog