Friday, December 4, 2015


Kamati kuu ya shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, imeidhinisha mageuzi yanayonuiwa kufufua hadhi ya shirikisho hilo lililokumbwa na kashfa nyingi.
Mapendekezo hayo yaliyoidhinishwa wakati wa mkutano wa kamati hiyo mjini Zurich inajumuisha sheria inayosema rais wa shirikisho hilo na maafisa wakuu wanaweza kuhudumu kwa kipindi cha miaka kumi
na miwili pekee na pia kuwepo kwa uchunguzi wa kina kuhusiana na maadili ya maafisa wa shirika hilo.
Uamuzi wa kuongeza idadi ya nchi zinazoshiriki katika fainali ya kombe la dunia kutoka 32 hadi 40 iliahirishwa hadi pale uchunguzi kuhusu athari zake utakapomalizika.

Mapendekezo hayo sasa yatawasilishwa wakati wa mkutano wa kamati kuu ya FiFA Februari mwaka ujao.
Awali maafisa wa polisi mjini Zurich waliwakamata manaibu wa rais wawili wa shirikisho hilo kama sehemy ya uchunguzi wao kuhusiana na madai ya ufisadi na hongo.
Polisi walifika katika hoteli ya kifahari ya Baur au Lac mjini humo na wakaonekana wakiondoka na watu wawili.
Shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limesema litashirikiana kikamilifu na wachunguzi.
Hii ni mara ya pilikwa hoteli hiyo inayotumiwa na maafisa wa Fifa kuvamia na polisi mwaka huu huku tuhuma za ufisadi zikiendeleakulizonga shirikisho hilo.
Mkutano wa siku mbili wa kamati tendaji ya Fifa unaendelea katika mji huo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog