Waswahili hawaishiwi vioja kwa tungo,
nahau, mafumbo, methali hata vitendawili. Yote yanaakisi maisha ya jamii
pana inayotuzunguka. Kwa leo nimeguswa na msemo usemao, nabii
hakubaliki kwao.
Nimesimama peke yangu nikiamini kuwa
wapo manabii ambao wanakubalika kwao. Utakubaliana nami kuwa kiwango
alichonacho Mbwana Samatta hakuna mtanzania asiyekikubali. Kwa sasa
Samatta ndiye chachu na roho ya Tp mazembe. Huwezi kumwambia kitu Moses
Katumbi juu ya kijana huyu wa kitanzania.
Anaibeba timu kwa uwezo wake baada ya
kuondoka Tresor Mputu aliyetimkia nchini Angola, sasa hakuna kama
Samatta . Ukipita kwenye viunga vya mji wa Lubumbashi vijana wanapendeza
kwa jezi ya Samatta. Timu yetu ya Taifa Stars jumapili hii iko dimbani
kucheza na timu ya Taifa ya Burundi. Ni siku ambayo nabii ata zidhirisha
unabii wake. Naamini sasa ni wakati wa Mbwana Samatta kuibeba Taifa
Stars.
Tanzania imejaliwa kuwa na vipaji
vingi katika medani mbalimbali, lakini kukosekana mipango thabiti na
uthubutu miongoni mwa wachezaji ni tatizo katika kupata wachezaji wa
kulipwa. Wenzetu Kenya wana nyota kadhaa wanaosukuma kandanda barani
Ulaya.
Kama vile kwa Waganda ambao nao hawako
nyuma, kwetu Samatta atabaki kuwa kioo cha taifa kwenye mpira wa miguu .
Mechi ya jumapili itaamuliwa na ubora wa Mbwana Samatta. Kila la heri
Taifa Stars kwenye mchezo huo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya
shirikisho la soka duniani Fifa. Uzalendo wetu ni silaha tosha ya
kuiangusha Burundi nyumbani kwao.
0 maoni:
Post a Comment