Friday, September 4, 2015



Kadri siku zinavyo zidi kwenda tuna anza kujua mambo mengi yaliyokuwa nyuma ya pazia la usajili wa vilabu mbalimbali barani Ulaya, vipo vilabu ambavyo vilikosa wachezaji kwa sababu ya dau na mengine mengi. Ila usajili uliyoshindikana kutimia ni Pedro Rodriguez kushindwa kujiunga Man United wakati kila kitu kilikuwa tayari.
Pedro-602777
Ed Woodward alisafiri hadi Barcelona Hispania ili kukamilisha usajili wa Pedro kujiunga na Man United ila klabu ya Chelsea ndio iliizidi kete Man United, licha ya awali kuripotiwa kukubali kujiunga na Man United kwa dau la pound milioni 21.
Habari kutoka katika vyombo vya habari vya Uingereza zinaripoti kuwa Pedro alisitisha mpango wa kujiunga na klabu ya Man United baada ya kuwasiliana na Victor Valdes na David De Gea, baada ya kuwasiliana na hao na walimwambia kuhusu tatizo la Van Gaal na wachezaji Pedro akabadili mawazo.
Barcelona-341349
“Ni kweli sikupenda walivyofanyiwa wachezaji wenzangu hususa kwa Victor ambaye nimewahi kucheza nae timu moja, aliniambia kuhusu Man United kuwa ni klabu nzuri na ina mashabiki wengi ila tatizo ni kocha, nilizungumza vizuri na uongozi wa klabu, lakini na amini nilifanya maamuzi sahii kujiunga na Chelsea”>>> Pedro

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog