Friday, September 4, 2015



Baada ya kuweka headlines nyingi usiku wa tuzo za MTV VMA’s mwaka huu na show iliyoisha kwa machozi, Justin Bieber kaamua kuzungumza sababu zilizompelekea kuangusha machozi akiwa katikati ya show yake  ya MTV VMA’s 2015 jijini Los Angeles Marekani.
Siku ya Jumatano msanii huyo wa R&B Pop alialikwa kwenye kipindi cha ‘The Tonight Show’ cha Jimmy Fallon kuzungumzia maisha yake,video yake mpya pamoja na tukio lililotokea usiku wa MTV VMA’s siku ya jumapili August 30.
Justin Bieber kwenye kipindi cha The Tonight Show siku ya Jumatano 04 September 2015.
>>>“Nilifurahi kupita kiasi, nimefanya utoto mwingi hapa kati kati na wala sikutegemea kama watu wangeonyesha support kubwa sana kwangu siku ile kwa sababu mara ya mwisho mimi kuperform kwenye show nilizomewa sana nikajisikia vibaya”. <<< Justin Bieber.
Justin Bieber alikiri kuwa alikuwa mkorofi bila sababu za msingi, aliwakwaza wengi na alichukulia vitu vingi sana poa kiasi cha yeye kusahau tarehe ya uzinduzi wa moja ya album zake hivyo alihisi kuwa akirudi jukwani watu hawatampokea vizuri na pengine wengi wanamchukia.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog