Friday, September 4, 2015

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa ameonge na vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya timu na hali za wachezaji siku moja kabla ya mechi dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Walitakiwa kuwepo makocha wa timu zote mbili ila kocha wa Nigeria Sunday Oliseh hakutokea.
Timu ya taifa ya Tanzania imefanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mechi dhidi ya Nigeria asubuhi ya Septemba 4 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, lakini wachezaji wote wapo fiti ila Mbwana Samatta amepata majeraha ya kawaida katika mazoezi.
“Wachezaji wapo vizuri ila aliyekuwa majeruhi serious ni Abdi Banda ambaye atakaa nje ya uwanja kwa siku 21 baada ya kuumia nyama za paja, Samatta amepata majeruhi ya kawaida asubuhi ya leo katika mazoezi ya mwisho ila hadi jioni atakuwa yupo sawa”>>> Mkwasa
Timu ya taifa ya Nigeria ambayo inanolewa na kocha mzawa kama ilivyo kwa Tanzania imewasili usiku wa Septemba 3 Uwanja wa ndege wa kimataidfa JKN Dar Es Salaam, ikiwa na kikosi cha wachezaji wake, ila kocha Sunday Oliseh hii itakuwa ni mechi yake ya kwanza toka aanze kuifundisha Super Eagles hivyo presha itakuwa pande zote mbili.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog