Friday, September 4, 2015





Nahodha mpya wa Uholanzi, Arjen Robben alitoka uwanjani baada ya dakika 27 tu kufuatia kuumia nyonga PICHA ZAIDI GONGA HAPA



TIMU ya taifa ya soka ya Iceland imejisogeza kukata tiketi ya kufuzu kucheza mchuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2016 baada ya ushindi wa penalti ya utata ya Gylfi Sigurdsson w 1-0 dhidi ya Uholanzi waliomaliza pungufu ya mchezaji mmoja usiku wa jana.

Refa Milorad Mazic wa Serbia, aliyemtoa kwa kadi nyekundu Martins Indi dakika ya 33, aliwazawadia mkwaju wa penalti Iceland dakika ya  51 ingawa Gregory van der Wiel alionekana kuuwahi moira wakati anapambana na Birkir Bjarnason. 

Sigurdsson akaenda kufunga penalti hiyo akimtungua kipa Jasper Cillessen na kuiweka Iceland katika mazingira mazuri ya kukata tiketi ya kwanza ya fainali za michuano mikubwa. 

Matokeo hayo yanaiweka Uholanzi katika mazingira magumu kidogo katika kundi hilo A kutokana na Iceland kutimiza pointi 18, mbili zaidi ya Jamhuri ya Czech wanaoshika nafasi ya pili. Uholanzi inabaki na pointi zake 10.

Iceland sasa wanaweza kujihakikishia kucheza Euro 2016 iwapo tu watashinda mchezo wa nyumbani dhidi ya Kazakhstan Jumapili.

Kipigo hicho kinamuweka pabaya kocha mpya wa Uholanzi, Danny Blind. Kocha aliyetangulia Guus Hiddink alilazimika kujiuzulu kwa sababu ya matokro mabaya hususan baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-0 nchini Iceland mwezi Oktoba.

Mshambuliaji Robin van Persie, ambaye aliiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil zaidi ya mwaka mmoja uliopita, jana aliwekwa benchi na kocha Blind. 


MECHI ZILIZOSALIA

Septemba 6; 
Latvia vs Jamhuri ya Czech Uturuki vs Uholanzi
Iceland vs Kazakhstan
Oktoba 10 
Iceland vs Latvia, Kazakhstan vs Uholanzi Jamhuri ya Czech vs Uturuki
Oktoba 13
Latvia vs Kazakhstan; Uholanzi vs Jamhuri ya Czech 
Uturuki vs Iceland

Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen, Van der Wiel, De Vrij, Martins Indi, Blind, Wijnaldum/Promes dk80, Klaassen, Robben/Narsingh dk31, Sneijder, Depay na Huntelaar/Bruma dk40.

Iceland; Halldorsson, Saevarsson, Arnason, Ragnar Sigurdsson, Ari Freyr Skulason, Bodvarsson/Finnbogason dk78, Gylfi Sigurdsson, Gunnarsson/Olafur Ingi Skulason dk86,Birkir Bjarnason, Gudmundsson na Sigthorsson/Gudjohnsen dk64).

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog