Friday, September 4, 2015


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametangaza kuwa ana $150,000 (£100,000) kwenye akaunti zake za benki, katika hatua inayolenga kupiga vita ufisadi katika nchi yake.
Kiasi hicho cha fedha kinaonyesha amekuwa akiishi ya kawaida sana tofauti na Makamu wake wa rais  Yemi Osinbajo ambaye ana utajiri wa kiasi cha $900,000 (£600,000) katika akaunti yake ya benki.
Rais huyo aliyeingia madarakani hivi karibuni anamiliki nyumba tano na mbili zikiwa za matope, pamoja na mashamba kadhaa.
Wakati akiingia madarakani aliwaahidi wananchi wake kukabiliana na ufisadi na kupambana na kundi hatari la Kigaidi la Boko Haram.
Taarifa zinasema ana shamba la matunda na ng’ombe 270, kondoo 25, farasi watano na ndege wengi.,Pia anamiliki hisa katika kampuni tatu.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog