Thursday, December 31, 2015

JANA Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ilibidi atulizwe munkari na Polisi ya kumpandishia Meneja mwenzake wa Sunderland Sam Allardyce wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Stadium of Light.
Klopp alipandwa na jazba wakati Jeremiah Lens wa Sunderland alipomchezea rafu mbaya Beki wa Liverpool Mamadou Sakho.
Wakati huo Liverpool walikuwa tayari washafunga Bao lao pekee na la ushindi kupitia Christian Benteke aliefunga Dakika ya 53.
Klopp aliamini Sakho ameumia vibaya na Lens alipaswa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu lakini Refa alimpa Kadi ya Njano.
Hapo ndipo Klopp alipoanza kumbatukia Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, na munkari ulipopanda Polisi waliingia kati kumtuliza Klopp.
Baadae, Allardyce alisema Klopp alitumia maneno mabovu na ya matusi na kumweleza Meneja huyo wa Liverpool kama 'Mjerumani laini'.
Hata hivyo, bifu halikuendelea kwani mwishoni Mameneja hao walipeana mikono kama ilivyo desturi Mechi ikimalizika.

Wednesday, December 30, 2015

LA LIGA: ..FC BARCELONA 4 v 0 REAL BETIS

Barcelona wamerejea tena kileleni mwa La Liga baada ya Timu za Jiji la Madrid, Real Madrid na Atletico Madrid, mapema kupokezana kukaa juu,
Barcelona, wakicheza kwao Nou Camp, waliitwanga Real Bertis 4-0 na kuongoza La Liga wakiwa na Pointi 38 kwa Mechi 16 wakifuata Atletico wenye Pointi 38 kwa Mechi 17 na Real wakiwa wa 3 na Pointi zao 36 kwa Mechi 17.
Bao za Barca zilifungwa na Westerman, aliejifunga mwenyewe katika Dakika ya 29, Lionel Messi, dakika ya 33 na Luis Suarez, Dakika za 46 na 83.
Mapema Leo, Real Madrid iliichapa Real Sociedad 3-1 na kutwaa uongozi.

Nao Atletico Madrid walibanwa na Rayo Vallecano hadi mwishoni ambapo Bao za Angel Correa, Dakika ya 88 na Antoine Griezmann, Dakika ya 90, ziliwapa ushindi wa 2-0.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog