Friday, December 20, 2013

Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
WABUNGE wamewataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu kutokana na maovu yaliyofanywa wakati wa Operesheni Tokomeza wakati wakijadili ripoti iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.

Baadhi ya wabunge waliochangia kuhusu kujiuzulu kwa mawaziri hao ni Mbunge wa Mwibara (CCM) Kangi Lugola, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Longido (CCM) Lekule Laizer.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog