Monday, May 4, 2015


Meneja wa Manchester United Loius van Gaal amemvua jukumu la kupiga Penati Robin van Persie baada ya Jumamosi kukosa kufunga Penati na Timu yake kuchapwa 1-0 na West Bromwich Albion.
Alipohojiwa ikiwa Van Persie ataendelea kuwa chaguo la kwanza la upigaji Penati, Van Gaal alijibu: "Hapana. Sasa ni mwisho."
Aliongeza: "Siku zote ni hivyo. Wayne Rooney alishawahi kukosa na ukikosa unarudi chini!"
Kipigo hicho ni cha 3 mfululizo kwa Man United kwenye Ligi Kuu England na hii ni mara ya kwanza tangu 2001 kuchapwa mara 3 mfululizo kwenye Ligi.
Van Persie, mwenye Miaka 31, alikuwa na nafasi ya kuisawazishia Man United walipokuwa nyuma kwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 63 la frikiki ya Chris Brunt iliyombabatiza Jonas Olsson na kutinga lakini Penati yake ya Dakika ya 74 iliokolewa na Kipa wa WBA Boaz Myhill.
Mechi inayofuata kwa Man United kwenye Ligi ni Jumamosi Ugenini huko Selhurst Park na Crystal Palace.
Man United wako Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya 5 Liverpool huku Mechi zikiwa zimebaki 5.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog