Monday, May 4, 2015


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinumz ambaye ni balozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania akiimba jukwaani Zari White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. App hiyo inawaletea wateja burudani ya muziki kiganjani. Picha zote na BAZIRA.COM


Mchumba wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinum... Bibie Zari the bossylady akiwashukuru Watanzania waliofika katika Zari White Party lililofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Umati wa Watanzania waliohudhuria katika Zari White Party lililofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mmoja ya vingozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania akitoa maelezo machache kwa wateja waliofika katika Zari White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. App hiyo inawaletea wateja burudani ya muziki kiganjani.
Msanii wa Kizazi Kipya, Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi akipozi katika zuria jekundu.

Msanii Shetta nae hakuwa nyuma kushow love mbele ya zuria jekundu.
Wafanyakazi wa Vodacom wakiwa amepozi katika zuria jekundu.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinumz ambaye ni balozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania akiwa amepozi na mkewe mtarajiwa Zari katika Zari White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Waliopo pembeni ni Madame Ritha, Msanii Ney Wa Mitego. Wengine ni Msanii A.K.A (kushoto) toka nchini Afrika Kusini.

---
Mziiki ni huduma ya muziki ya Afrika ambayo inatoa huduma hiyo kwa muziki wa kitaifa na kimataifa, inajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa sehemu ya wadhamini wa pati ya Zari All-White party iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mziiki ni sehemu ya kuendeleza wasanii wa ndani na nje ya Afrika ambapo watumiaji wa simu za smartphones za Android, iOS na BlackBerry wanapata nafasi ya kusikiliza nyimbo mbalimbali kwa kupitia simu zao za mkononi.Wateja wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kutumia intaneti ya wi-fi wanaweza kuperuzi na kupata nyimbo ambazo wanaweza pia kuziweka katika miito yao ya simu pia kuzisambaza kwa rafiki zao bure kwa kipindi cha mwezi mzima ambao ni ofa.

Huduma hii inapatikana katika vifurushi vyote vya Lite na Premium, na huduma ya Lite inapatikana pia kwa watumiaji wote wa mtandao wa wi-fi ambao wanaweza pia kuperuzi moja kwa moja bila malipo yoyote kila mahali mtandao wa Vodacom unapopatikana. Tangu Mziiki izinduliwe mwezi Mei mwaka jana, imefanikiwa kuingiza zaidi ya wasanii 1000 wa Afrika ambao wanafanya vizuri mpaka sasa.

Huduma hii imechaguliwa sana kwa ajili ya kuhakikisha Waafrika wanafurahia muziki wao ambapo inaendelezwa na Spice Africa, na ilianzia Tanzania lakini kwa sasa inazidi kukua katika nchi mbalimbali.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Spice Africa, Arun Nagar, alisema ‘Huduma ya hii ya kidijitali inalenga zaidi kuibua vipaji katika nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara Afrika ambapo pia ni nafasi nzuri kwa wasanii mbalimbali kutangaza kazi zao’.

‘Tunajivunia kuwa sehemu ya wadhamini wa sherehe za Zari-White Party ambapo pia tuna imani kuwa Watanzania wengi watazidi kufurahia huduma zetu’ Nagar aliongeza kuwa Mziiki ni huduma ambayo inapatikana kirahisi mno kwa kutumia simu za mkononi kwa kupata huduma ya muziki wa wasanii wa ndani na nje ya Afrika.

Diamond Platnumz, ambaye ni balozi wa Mziiki Tanzania, alisema ‘Mziiki imekuwa katika nafasi ya kutoa kipaumbele kwa wasanii mbalimbali kwa ajili ya kupata changamoto kwa wasanii wakubwa kitaifa na kimataifa’ “Muziki wetu umezidi kufanya vizuri katika nchi mbalimbali, na Mziiki inatoa ofa kwa wadau mbalimbali wa muziki kusikiliza nyimbo wanazozipenda kwa kupitia katika viganja vyao,” alisema Diamond Platnumz.

Burudani mbalimbali zilizotolewa katika sherehe hizo za Zari White Party ikiwa ni pamoja na muziki kutoka kwa DJ, muziki wa live kutoka kwa wasanii kama vile Diamond Platnumz na Shetta wakati msanii mwalikwa atakua AKA, kutoka Afrika Kusini.

Zari All-White Party 2015 imedhaminiwa na Vodacom na Mziiki kwa kushirikiana na SK Entertainment, Clouds Entertainment, Prime Time Promotions, Johnny Walker Gold label ( Serengeti Breweries) ambapo ilianza The All-White Parties mwaka 2009 nchini Uganda na Tanzania inafanyika mwaka huu kwa mara ya kwanza.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog