Thursday, October 15, 2015


www.bukobasports.comFIFA imethibitisha kuwa inachunguza Uhamisho wa Eliaquim Mangala kutoka FC Porto kwenda Manchester City kutokana na kukiukwa kwa Sheria zinazokataza Mchezaji kumilikiwa na pande tatu.
Mangala, Mchezaji wa Kimataifa wa France, ameichezea Man City mara 31 kwenye Ligi Kuu England tangu ahamie hapo kutoka Porto Agosti 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 32.
Imedaiwa kuwa Kampuni iitwayo Doyen Sports, yenye Ofisi zake Nchini Malta na Jijini London, ililipa Pauni Milioni 2 Mwaka 2011 ili kununua Hisa za Umiliki wa Mchezaji huyo wakitegenea thamani yake itapanda.
Inasemekana baada ya City kumnunua Mangala kutoka Porto, Doyen Sports ililipwa Pauni Milioni 10.6 kama mgao wao wa mauzo ya Mchezaji huyo.
Ikiwa uchunguzi wa FIFA utabaini kuna ukiukwaji wa Sheria basi FC Porto, na si Man City, ndio watakaoadhibiwa kwa kupigwa Faini au kufungiwa Kuuza au Kununua Wachezaji.
Mangala alianza Soka lake kwenye Chuo cha Soka cha Klabu ya Belgium Namur na kisha kuchukuliwa na Standard Liege akiwa na Miaka 17 ambako alicheza Mechi Zaidi ya 100 kwa Timu ya kwanza na kisha kujiunga na Porto.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog