Thursday, October 15, 2015


BAADA ya kupisha Mechi za Kimataifa kwa Wiki mbili, La Liga ipo dimbani Wikendi hii kwa Jumamosi kupigwa Mechi 5, Jumapili 4 na Jumatatu moja.
Vinara wa Ligi hii ya Spain ni Villareal ambao wako Pointi 1 mbele ya Timu 3 ambazo ni Real Madrid, Celta Vigo na Barcelona ambazo zote zimefungana zikiwa na Pointi 15 kila mmoja na kupishana tu kwa ubora wa Magoli.
Jumamosi Real Madrid wako kwao Santiago Bernabeu kucheza na Levante katika Mechi ya kwanza ya La Liga Wikiendi hii na Usiku Barcelona wataingia Uwanjani kwao Nou Camp kucheza na Rayo Vallecano.
Vinara Villareal wao wapo Nyumbani Jumapili kucheza na Timu ya 3 Celta Vigo.

LA LIGA
RATIBA
Jumamosi Oktoba 17

17:00 Real Madrid v Levante
19:15 Eibar v Sevilla
21:30 Barcelona v Rayo Vallecano
23:00 Valencia v Malaga
23:05 Real Betis v Espanyol

Jumapili Oktoba 18
13:00 Villarreal v Celta Vigo
17:00 Real Sociedad v Atletico Madrid
19:15 Getafe v Las Palmas
21:30 Deportivo v Athletic Bilbao

Jumatatu Oktoba 19
21:30 Sporting Gijon v Granada

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog