Tuesday, April 4, 2017



Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Ghent nchini Ubelgiji wamegundua njia mpya ya kutengeneza mafuta ya kuendeshea gari kwa kutumia majani ‘Biofuel’ ambapo kwa mujibu wa wanasayansi hao, majani yana uwezo wa kutengeneza kiwango kikubwa cha ‘decane’ ambacho hutumika katika kuzalisha mafuta.
Akizungumza na Science Daily, Professa Way Cern Khor alisema: >>> “Majani yamekuwa yakitumika kulisha wanyama lakini pia yanaweza kuzalisha mafuta ‘Biofuel’ kwa kiasi kikubwa. Hii inaweza kuja kusaidia kupunguza bei ya mafuta. Tunafurahi kuweza kubadilisha kitu kisichotumika na kuwa nishati muhimu.”
Prof. alielezea jinsi atakavyoweza kuyabadilisha majani na kuwa mafuta ya gari akisema kuwa majani hayo yatawekwa bakteria maalum watakaoweza kuondoa sukari iliyopo ndani yake na kubadilika kuwa katika asidi ya lactic na caproic ambayo inatumika kutengeneza mafuta.
Hadi sasa wanasayansi hao wameweza kutengeneza kiasi kidogo cha mafuta kinachotokana na majani lakini jitihada zinaendelea kuweza kubadilisha majani kuwa katika hali ya kimiminika.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog