Klabu
ya Spain, Sevilla, Jumatano wanawania kuweka Historia ya kuwa Klabu ya
kwanza kutwaa Kombe la EUROPA LIGI kwa mara ya 4 watakapokuwa ndani ya
National Stadium Mjini Warsaw, Poland, kucheza Fainali na Klabu ya
Ukraine, FC Dnipro Dnipropetrovsk.
Sevilla wametwaa Kombe hili mara 3 katika Miaka ya 2006, 2007 na 2014.
Mbali ya kuwania kuwa Klabu ya kwanza kulibeba Kombe mara 4, Sevilla pia wanawania kulitwaa ili kuweza kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao kwani, kwa mara ya kwanza, Bingwa wa EUROPA LIGI anaingizwa UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao.
Hii ni nafasi pekee kwa Sevilla ambao hivi Juzi walimaliza La Liga wakiwa Nafasi ya 5 na hivyo kukosa kuingizwa UEFA CHAMPIONS LIGI.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dnipro kucheza Fainali ya Klabu Barani Ulaya.
Sevilla, chini ya Kocha Unai Emery, wamefika Fainali hii kwa kuzitoa Borussia Monchengladbach, Villarreal, Zenit St Petersburg na Nusu Fainali Fiorentina ambayo waliinyuka Jumla ya Mabao 5-0 na hiyo yote ni kutokana na kazi njema ya Wachezaji wao kina Carlos Bacca, Aleix Vidal, Kevin Gameiro na Jose Antonio Reyes.Dnipro, chini ya Kocha Myron Markevych na kwa mshangao wa wengi, wametinga Fainali kwa kuzibwaga Olympiakos, Ajax, Club Brugge na kisha Napoli kwenye Nusu Fainali baada ya kutoka 1-1 katika Mechi ya Kwanza huko Italy na kushinda 1-0 katika Marudiano kwa Bao la Yevhen Seleznyov.

0 maoni:
Post a Comment