Sunday, October 11, 2015


Wales wamefanikiwa kutinga Fainali yao ya kwanza ya Mashindano makubwa tangu Mwaka 1958 baada ya Jana kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, licha ya kuchapwa 2-0 Ugenini na Bosnia.
Wales wamefuzu kutoka Kundi B la EURO 2016 pamoja na Belgium ambao Jana waliinyuka Andorra 4-1 kutokana na Cyprus kuichapa Israel 2-1 katika Mechi nyingine ya Kundi hilo.
Italy nao wamefuzu kutoka Kundi H baada ya kushinda Ugenini walipoichapa Ugenini Azbeijan Bao 3-1.
Hadi sasa Timu 12, pamoja na Wenyeji France, zimeshatinga Fainali za EURO zikibakisha Nafasi 12 ambazo 8 zitajazwa kwa Mechi kati ya Leo na Jumanne na 4 zitatokana na Mechi 4 za Mchujo zikishirikisha Washindi wa 3 Bora wa Makundi ambazo zitachezwa Mwezi Novemba.
Kutoka Kundi A, hali ni tete kwa Netherlands ambao Jana waliifunga Ugenini Kazakhstan 2-1 lakini wapo hatarini kuikosa Nafasi ya 3 kwa vile Turkey nao walishinda Ugenini kwa kuichapa Czech Republic 2-0.

Toka Kundi A, Iceland na Czech Republic tayari zimefuzu na nafasi inayogombewa ya kwenda Fainali ni kupitia Tiketi ya Mshindi wa 3 ambayo Turkey watainasa wakitoka Sare na Iceland huko Uturuki Jumanne.
Bao za Holland hapo Jana zilifungwa na Georginio Wijnaldum na Wesley Sneijder huku Straika wa zamani wa Manchester United akiingizwa Kipindi cha Pili kuichezea Holland Mechi yake ya 100.


Katika Mechi ya mwisho hapo Jumanne, Holland watakuwa Wenyeji wa Czech Republic.

 
TIMU ZILIZOFUZU HADI SASA [9 bado 15]:
-France [Wenyeji]
-KUNDI A: Iceland, Czech Republic
-KUNDI B: Belgium, Wales
-KUNDI C: Spain
-KUNDI D:
-KUNDI E: England, Switzerland
-KUNDI F: Northern Ireland
-KUNDI G: Austria
-KUNDI H: Italy
-KUNDI I: Portugal
EURO 2016
RATIBA
Saa za Bongo
Jumapili Oktoba 11
1900 Armenia vs Albania
1900 Faroe Islands vs Romania
1900 Finland vs Northern Ireland
1900 Greece vs Hungary
1900 Serbia vs Portugal
2145 Germany vs Georgia
2145 Gibraltar vs Scotland
2145 Poland vs Republic of Ireland
Jumatatu Oktoba 12
1900 Austria vs Liechtenstein
1900 Russia vs Montenegro
1900 Sweden vs Moldova
2145 Belarus vs Macedonia
2145 Estonia vs Switzerland
2145 Lithuania vs England
2145 Luxembourg vs Slovakia
2145 San Marino vs Slovenia
2145 Ukraine vs Spain
Jumanne Oktoba 13
2145 Belgium vs Israel
2145 Bulgaria vs Azerbaijan
2145 Cyprus vs Bosnia and Herzegovina
2145 Italy vs Norway
2145 Latvia vs Kazakhstan
2145 Malta vs Croatia
2145 Netherlands vs Czech Republic
2145 Turkey vs Iceland
2145 Wales vs Andorra

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog