Sunday, October 11, 2015


Timu ya Taifa ya Tanzania Leo hii inajitupa Uwanja wa Kamuzu Banda huko Blantyre kurudiana na Wenyeji Malawi katika Raundi ya Kwanza ya Kanda ya Afrika ya Mchujo wa Kombe la Dunia ambazo Fainali zake zitafanyika huko Russia Mwaka 2018.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Jumatano iliyopita Tanzania iliichapa Malawi 2-0 kwa Bao za Maprofeshanali Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wote hucheza huko Congo DR kwenye Klabu ya Lubumbashi TP Mazembe.
Kikosi cha Tanzania huko Malawi kipo chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa.
Ikiwa Tanzania watafanikiwa kuvuka kigingi hiki cha Malawi basi kwenye Raundi ya Pili watavaana na Algeria ambao wanaanzia hatua hiyo.
Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja.



KOMBE LA DUNIA 2018
RATIBA:
Afrika-Raundi ya Awali- Marudiano
Jumapili Oktoba 11

15:00 Malawi v Tanzania [0-2]
16:00 Ethiopia v Sao Tome And Principe [0-1]
16:00 Kenya v Mauritius [5-2]

Jumanne Oktoba 13
14:30 Madagascar v Central African Republic [3-0]
16:00 Burundi v Seychelles [1-0]
17:00 Sierra Leone v Chad [0-1]
18:00 Namibia v Gambia [1-1]
18:00 Niger v Somalia [2-0]
19:00 Lesotho v Comoros [0-0]
19:00 Guinea-Bissau v Liberia [1-1]
20:00 Botswana v Eritrea [2-0]
20:00 Swaziland v Djibouti [6-0]
20:00 Mauritania v South Sudan [1-1]

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog