Nemanja Vidic akipata picha ya pamoja na Sir Bobby Charlton kwenye uwanja wa Old Trafford leo wakati Man United walipoikaribisha timu ya Hull City
Kwaheri kijana!!! Nemanja anatimkia kucheza soka lake la mwisho huko Inter Milan
Vidic na baadhi ya wachezaji wa United
Vidic alianzia benchi kwenye mtanange wao na Hull City ambapo Vidic alichukua nafasi ya Phil Jones baada ya kuumia bega akiwa kwenye patashika za hapa na pale wakati wa kona.
Pia, Meneja-Mchezaji, Ryan Giggs, ambae aliingia kucheza Kipindi cha Pili na ambae ndie alitoa Pasi yenye akili iliyompa mwanya Robin van Persie, huenda nae pia ikawa hii ndio Mechi yake ya mwisho Old Trafford kama Mchezaji kwa vile Mkataba wake nae kama Mchezaji unamalizika mwishoni mwa Msimu.
Man United wamebakiza Mechi moja ya Ligi hapo Jumapili ambako watacheza Ugenini kwa Mtakatifu Maria dhidi ya Southampton na ushindi kwao na kipigo kwa Tottenham kitawapa Nafasi ya 6 na hivyo kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao.
0 maoni:
Post a Comment