Tuesday, September 22, 2015

MABINGWA wa Bundesliga Bayern Munich na Vinara wa Ligi hiyo Borussia Dortmund wana Mechi ngumu za Ligi hiyo ya Germany Leo Jumanne na Jumatano Usiku.
Jumanne, Bayern Munich wako kwao Allianz Arena kucheza na VfL Wolfsburg ambao wako Nafasi ya 3 baada ya kushinda Mechi 3 na Sare wakiwa na Pointi 11 zikiwa ni Pointi 4 nyuma ya Bayern ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 15 sawa na Vinara Borussia Dortmund.
Msimu huu, Wolfsburg, ambao ndio waliobeba German Cup, walishaifunga Bayern Munich Mwezi Agosti baada ya kuwabwaga kwa Penati kwenye Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya ya kugombea Super Cup.
Nao Borussia Dortmund Jumatano wapo Ugenini kucheza na Hoffenheim wakisaka ushindi wao wa 6 mfululizo kwenye Bundesliga.
BUNDESLIGA
RATIBA
Jumanne Septemba 22

21:00 Bayern Munich v VfL Wolfsburg
21:00 Hertha Berlin v Cologne
21:00 Ingolstadt v Hamburg
21:00 Darmstadt 98 v Werder Bremen
Jumatano Septemba 23

21:00 Schalke 04 v Eintracht Frankfurt
21:00 Bayer Leverkusen v Mainz
21:00 Borussia Moenchengladbach v Augsburg
21:00 Hanover 96 v VfB Stuttgart
21:00 Hoffenheim v Borussia Dortmund

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog