Wednesday, July 30, 2014


r
Nyota anayewindwa: Msimu uliopita, Lukaku alifunga mabao 15 akiwa na klabu ya Everton ambayo inakaribia kumsajili kwa mkataba wa kudumu.

Romelu Lukaku atakamilisha uhamisho wa kujiunga na Everton kwa dau la paundi milioni 24 baada ya kutangaza kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twita mchana wa leo akisema: Ni muda wa kuanza ukurasa mpya.

Inafahamika kuwa nyota huyo mwenye miaka 21, ambaye msimu uliopita alikipiga Goodison Park kwa mkopo atasaini mkataba wa miaka mitano na Everton na kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji aliyeiwakilisha nchi yake katika fainali za mwaka huu za kombe la dunia nchini Brazil, amekuwa akihusishwa kuondoka darajani majira yote ya kiangazi mwaka huu.
Everton ameamua kumpa mkataba wa kudumu baada ya kuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao 15 msimu uliopita.
Roberto Martinez ameamua kuvunja rekodi ya dau la usajili la klabu ambapo dau alilosajiliwa Marouane Fellaini la paundi milioni 15 lililokuwa linashikilia rekodi.
Nafasi ya Lukaku katika klabu yake ya Chelsea ingefinywa zaidi na Diego Costa, Fernando Torres na Didier Drogba aliyesajiliwa siku za karibuni.
Hii ni taarifa njema kwa mashabiki wa Eberton ambao jana walimshuhudia Ross Barkley akijifunga mkataba wa miaka minne Goodison Park.
View image on Twitter

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog