Marafiki: Nemanja Vidic akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck.
Nemanja Vidic amefichua siri kuwa
alipata ofa nyingi baada ya kutangaza maamuzi ya kuondoka Manchester
United, ikiwemo klabu za England.
Mserbia huyo alitangaza maamuzi ya kuondoka Old Trafford mwezi februari mwaka huu baaada ya kucheza kwa miaka 8.
Vidic alikubali kujiunga na Inter Milan mwezi machi mwaka huu kufuatia mkataba wake kumalizika majira ya kiangazi mwaka huu.
Katika mohajiano yaliyojaa hisia na
MUTV kueleka mchezo wa jana baina ya Man United na Inter mjini
Washington D.C., ambapo United walishinda kwa penalti 5-3, beki huyo
alisema: 'Nilikuwa na ofa nyingi kutoka mataifa tofauti, hata kutoka
England. Inter ipo wakati wa mpito, inajitahidi kujiimarisha, lakini
nimependa mpango wao. Inter itakuwa kubwa na kubwa zaidi , naamini
nitawasaidia kufikia malengo yao".
Vidic akimuonesha ufundi mchezaji mwenzake wa zamani wa Man United, Danny Welbeck.
Vidic ambaye mara nyingi anapenda
kutumia neno 'sisi' kila anapoizungumzia United, pia anaamini klabu yake
ya zamani itaimarika zaidi chini ya kocha Louis Van Gaal baada ya
kutimuliwa kazi kwa David Moyes.
"Ikiiangalia klabu kwa sasa, ipo wakati
wa mpito. Wachezaji wapya wanaingia, Sisi (United) tumebadili makocha,
wa kwanza David Moyes na sasa Louis Van Gaal na hata mkurugenzi
alibadilishwa baada ya mwaka jana David Gill kuondoka na ( Ed Woodward
alipandishwa)'
'Natumaini mwaka huu ni muhimu kwao na
wachezaji waliosubiri nafasi watapata nafasi ya kuingia kikosini.
Wachezaji wapo tayari kwa nafasi".
0 maoni:
Post a Comment