Sam
Mapenzi (katikati) akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band ndani
ya fukwe za Escape One katika show maalum kwa ajili ya kusheherekea
sikukuu ya Eid-El Fitr huku akipewa back Vocal na Sony Masamba pamoja na
Aneth Kushaba AK47.
Aneth
Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani kuwapa raha mashabiki wa Skylight
Band katika kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwenye ukumbi wa Escape
One.
Mashabiki wa Skylight Band mdogo mdogo wakiachia kwenye dancing floor.
Sam
Mapenzi akitoa burudani adimu mashabiki wa Skylight Band katika sikukuu
ya Eid El Fitr kwenye kiota cha Escape One jijini Dar.
Skylight Band ni #balsaa# hebu angalia mashabiki wanaojua burudani ya muziki wa Live wanavyosebeneka.
Rappa
Mkongwe Joniko Flower akitunzwa wekundu wa msimbazi na mmoja wa
mashabiki wa Skylight Band aliyekunwa na uimbaji wa rapa huyo.
Binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni Mary Lucos akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani).
Mary Lucos wa Skylight Band akiwaduarisha mashabiki wa bendi hiyo katika sikukuu ya Eid El Fitr ndani kiota cha Escape One.
Wadada wakijipinda kuzungusha nyonga zao.
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiduarika.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya umati wa wakazi wa Dar wake kwa waume
waliokusanyika ndani ya fukwe za Escape One kujipatia upepo mwanana huku
wakiburudishwa na Skylight Band.
Mashabiki
wa Skylight Band wakiendelea kuburudika na vinywaji mbalimbali huku
wakisiliza burudani ya kutoka bendi ambayo kwa sasa ndio habari ya
mujini.
Ale Mama mupe Saluti……!!! Twende kazi…..
Muguu
wa kushoto mbele wa kulia nyuma….Yachuma chuma…!! Kikosi cha Skylight
Band wakicheza sambamba na mashabiki wao katika kusheherekea sikukuu ya
Eid El Fitr kwenye kiota cha Escape One.
Burudani ikiendelea na watu wakiendelea kusebeneka.
Wadada walichizikaje…!?
Pichani
juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakionyesha umahiri wao wa
kucheza moja ya staili za bendi hiyo kwa wanamuziki Joniko Flower na
Sony Masamba.
Daudi
Tumba akitweta jasho kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata
ladha nzuri ya muziki kupitia ala za Band hiyo huku Tumba ikihusika pia
kutengeneza sauti nzuri kabisa.
Pichani juu na chini ni Hashim Donode a.k.a Mzee wa Viduku akifanya yake!
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Skylight Band, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana
mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bendi hiyo Justine Ndege wakati
Skylight Band ikiendelea kutoa burudani kwenye sherehe za sikukuu ya Eid
-El- Fitr ndani ya kiota cha Escape One.
Blogger
William Malecela a.k.a LEMUTUZ mwandaaji wa Instagram Party
itakayofanyika Jumamosi hii kwenye kiota cha Escape One akishow love na
Fans wake mdau Joseph Magige.
Sam Mapenzi kwenye ukodak na Customer care huku akionyesha Video mpya ya “Pasua Twende” kupitia simu yake ya kiganjani.
Emma Bass wa Skylight Band (kulia) akipata ukodak na swahiba wake.
Joniko Flower wa Skylight Band akishow love na mdau.
Mratibu wa Skylight Band Lubea akipata ukodak na Mwimbaji Mary Lucos back stage.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Skylight Band na Rais wa #WANAMANYOYA# Justine Ndege
(katikati) akipata Ukodak Mkuu wa Itifaki wa #WANAMANYOYA# Eddie Viede
pamoja na mdau wa Skylight Band James Rock Mwakibinga.
Palinogaje wewe tu umekosekana….Si haba kesho pia ni siku tukutane viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
Aneth Kushaba AK 47 a.k.a Komando Kipensi akishow love na Tophy mpiga bass wa Skylight Band back stage.
0 maoni:
Post a Comment