Wednesday, January 29, 2014



Wabunge wa Ukraine
Bunge la Ukraine limeidhinisha sheria inayotoa msamaha kwa waandamanaji waliozuiliwa wakati wa vurugu zilikumba taifa hilo katika siku za hivi karibuni.
Vyama vya upinzani vilisusia kura hiyo kulalamikia kifungu katika mswada wa sheria hiyo ambacho kinasema msamaha utatolewa tu ikiwa waandamanaji watasalimisha majengo ya serikali ambayo wameteka katika siku za hivi karibuni.
Waandamanaji katika baarabara za mji mkuu wa Kiev kadhalika wamekatalia mbali hatua hiyo.
Maandamano hayo yalianza mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya rais Viktor Yanukovych kubatili uamuzi wa kusaini mkataba wa kibiashara kati ya Ukraine na umoja wa ulaya.
Kisha baadaye akatia saini mkataba wa mkopo wa takriban dola bilioni 15 na Urusi.
Maandamano bado yanaendelea nchini Ukraine
Hapo jana jumatano, mkuu wa sera za za kigeni katika umoja wa Ulaya Catherini Ashton alisema kuwa amegutushwa na vurugu zilizosababisha maafa katika mji wa mkuu wa Kiev na maneo mengine ya taifa hilo.
" Ni lazima nisema kuwa nimegutushwa sana anasema Bi. Ashton, na ripoti na ripoti ambazo nimepata kuhusu hali ilivyo na bila shaka mojawepo wa maswala muhimu tunayopaswa kushugulikia ni kuzuia vurugu na vitisha. Nina wasiwasi kuhusu watu ambao inaonekana wametoweka. Kuna gumzo kali kwamba ukijadili hili na watu wengi, kuhusu watu kuwa katika hali iliyo sawa na mateka na mengine yanayotokana na vurugu ni sharti yakome. Ni swala lenye umuhmu mkubwa,'' anasema Bi Catherine Ashton
Catherine Ashton - ambaye yuko mjini Kiev kufanya mazungumzo na bwana Yanukovych pamoja na makundi ya upinzani amesema Ukraine inahitaji suluhu ya kisiasa itakayopatikana kwa haraka na kumshirikisha kila mmoja.
Hapo jana jioni mswada huo wa kutoa msamaha ulipitishwa kwa kura 232 dhidi ya 11, huku chama cha Bwana Yanukovych cha Party of the Regions kilicho na idadi kubwa ya wabunge kikiunga mkono.
Lakini wabunge 173 hawakupiga huku wabunge wa upinzani wakipiga mayowe kupinga kura hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog