Wednesday, November 25, 2015


Kwa mara nyingine tena kocha wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Louis van Gaal amekiri kikosi chake kuhitaji winga mwenye kasi, kitu ambacho kilianza kuibua upya zile fununu za kutaka kumsajili winga wa kimataifa wa Uholanzi anayeichezea klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Arjen Robben.
Kocha wa Man United Louis van Gaal anahusishwa kutaka kumsajili Arjen Robben ambaye amewahi kumfundisha winga huyo miaka kadhaa wakati akiwa kocha wa FC Bayern Munich na sasa, anatajwa kutaka kusajili winga mwenye kasi kitu ambacho kilifanya aulizwe kama Robben yupo kwenye mipango yake kama ilivyoripotiwa wiki iliyopita?
Arjen-Robben-Wallpaper-HD-86563
“Nahitakji kubalansi kikosi changu ni kweli tunahitaji winga mwenye kasi kwani tunahitaji kuwa nafasi nzuri niliyopanga tuwepo, kuhusu kumuhitaji Robben siwezi kujibu swali hilo kwani kama nitasema ‘milango ipo wazi kwa Robben’ najua utaenda kuandika tofauti na nilivyozungumza hivyo hilo sijibu” >>> Louis van Gaal
Wiki iliyopita mitandao mingi ya habari za michezo iliandika stori za Arjen Robben kuwa yupo katika mipango ya kuhamia Man United wakati wa dirisha dogo la usajili la mwezi January kwa uhamisho wa pound milioni 50 akitokea klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani ila kauli ya Van Gaal inaashiria dalili za kuwa upo uwezekano wa mpango huo.
van-gaal-hugging-robben

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog