Wednesday, November 25, 2015


Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kuwa wagumu wa kutumia fedha nyingi katika kuwekeza kununua wachezaji na kuboresha kikosi chake, Wenger mara nyingi majina ya wachezaji wakubwa na wanaouzwa kwa gharama za juu huwa anashindwa kuwasajili na mwisho wa siku wanasajiliwa na timu nyingine.
November 25 kauli ya kocha wa Arsenal Arsene Wenger imeingia katika headlines baada ya kuulizwa swali na muandishi kutokana na mwenendo wa tabia yake ya matumizi ya fedha hususani tukiwa tunaelekea katika dirisha dogo la usajili la mwezi January, hakubaliani na watu wanaomuita yeye bahili.
arsene-wenger-manages-a-smile-pic-getty-89992389
“Hapana sikubaliani na wewe kuwa mimi mbahili kama nitapata nafasi ya kukutoa out ndio utakapojua namna ambavyo huwa napenda kutumia fedha, rafiki zangu huwa hawanifirii hivyo, kwa sasa tunaenda kucheza na Olympiacos na tunaamini tutafuzu hatua ya 16 bora ya UEFA” >>> Arsene Wenger
Wenger usiku wa November 25 alifufua matumaini ya kikosi chake kusonga mbele katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya baada ya kufanikiwa kuifunga klabu ya Dinamo Zagreb kwa jumla ya goli 3-0, hivyo  matumaini ya kwenda hatua inayofuata yapo endapo watafanikiwa kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Olympiacos.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog