Anataka zaidi? Paul Pogba (kulia) atalipwa paundi elfu 23 kwa wiki kwa wakati huu katika klabu yake ya Juventus
LIGI ya Italia imeshuka umaarufu wake
ukilinganisha na ligi nyingine za ulaya na hii inatokana na mishara ya
wachezaji wa Seria A iliyotangazwa jumatatu ya wiki hii.
Daniele de Rossi
ndiye mchezaji anayelipwa zaidi ambapo anachukua paundi laki moja kwa
wiki na Gonzalo Higuain anamfuatia kwa kulamba paundi elfu 84 kwa wiki
na wa tatu ni Carlos Tevez anayepokea paundi elfu 70 kwa wiki.
Kwa mujibu wa gazeti la Gazzetta dello Sport,
klabu za Serie A kwa sasa zinatumia karibia paundi milioni 500 kwa
ajili ya malipo ya mishahara wa wachezaji chini ya kiwango cha mwaka
2011 na wachezaji wanaolipwa zaidi wanachukua hela ndogo ukilinganisha
na wachezaji nyota wa ligi kuu England na La Liga.
Kwa mfano, Paul Pogba, anapokea paundi
elfu 23 kwa wiki msimu huu licha ya kuwa miongoni mwa vijana wenye
kiwango cha juu duniani na katika klabu yake ya Juventus.
Juventus, ndio klabu inayoongoza kutumia
kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya mishara na ni klabu pekee ya
Italia ambayo inaongeza mishahara ya wachezaji kutoka 2013/2014 ambapo
Carlos Tevez na Arturo Vidal sasa wanapokea zaidi ya paundi elfu 60 kwa
wiki.
Nyota wa Roma, Daniele De Rossi ndiye
analamba mkwanja mrefu katika mkataba wake wenye thamani ya paundi
milioni 5.2 bila kujumuisha posho.
Nyota wa zamani wa Cheslea na sasa Roma
Ashley Cole aliamua kwenda Italia baada ya kutoongezewa mkataba Chelsea
na amesaini mkataba atakaomfanya apokee paundi elfu 35 kwa wiki katika
kikosi hicho cha Rudi Garcia.
Pesa ndefu: Nyota wa zamani wa Manchester City, Carlos Tevez (kushoto) ndiye analipwa zaidi katika klabu ya Juventus
Mpenda soka: Ashley Cole (kulia) aljiunga na Roma na analamba paundi elfu 35 kwa wiki
0 maoni:
Post a Comment