Sunday, July 19, 2015


MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amemuudhi Meneja mwenzake wa Everton baada ya kutangaza kuwa Chelsea imetoa Ofa ya kumnunua Beki John Stones.
Ofa hiyo ya kumnunua Beki wa Miaka 21 ya Pauni Milioni 20 imekataliwa na Everton.
Akiongea na Sky Sports News, Mourinho alisema: "Tumetoa Ofa kwa sababu tunampenda Beki huyo."
John Stones, ambae ameichezea England mara 4, alinunuliwa na Everton kutoka Barnsley Mwaka 2013 kwa Pauni Milioni 3.
Hata hivyo, kitendo cha Mourinho kutangaza waziwazi Ofa yao kimemkera mno Meneja wa Everton Roberto Martinez ambae alizungumza Jana huko Singapore mara baada ya kufungwa 3-1 na Arsenal kwenye Fainali ya Barclays Asia Trophy.
Martinez alisema: "Inasikitisha kwa Klabu kutamka hadharani. Sidhani kama sisi tunaweza kufanya hivyo na kuzumngumzia kuhusu Mchezaji. Joh Stones ni Mchezaji wa Everton, mwisho!"

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog