Friday, February 21, 2014


Nchini Tanzania michuano ya kusaka ubingwa wa ligi kuu ya nchi hiyo inaingia mzunguko wa 19 jumamosi hii kwa mechi tano, zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa nyumbani uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kumenyana na Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, Nayo Kagera Sugar ya Kaskazini magharibi mwa nchi hiyo inaikaribisha Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mjini Morogoro kutakuwa na mpambano kati ya Mtibwa Sugar na Ashanti United, wakati Coastal Union ya Tanga itaumana na timu ngeni na ngumu katika ligi hiyo-Mbeya City katika mechi itakayopigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Kikosi cha maaskari jeshi wa Oljoro JKT watakuwa nyumbani kupambana na Askari wenzao Mgambo Shooting katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha.
Jumapili hii itakuwa zamu ya mabingwa wa Zamani wa ligi hiyo, Simba watakao umana na JKT Ruvu, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku Mechi kati ya Azam Fc na Tanzania Prisons ikichezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog