Saturday, August 16, 2014

 

Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila akipunga mkono baada ya kutawazwa kuwa malkia wa Kanda ya Kinondoni katika shindano lililoshirikisha wanyange 16 waliokuwa wakiwania tiketi ya  kushiriki shindano la Miss Tanzania 2014. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo. 

Shila ameungana na warembo wengine Camila Cindy John aliyeshika nafasi ya pili na Queenlatifa Hashim aliyeshika nafasi ya tatu ambao kwa pamoja wamepata tiketi ya kuiwakilisha Kanda ya Kinondoni katika mashindano ya taifa ya Miss Tanzania 2014 yanayotaraji kufanyika mapema mwezi Oktoba.
  Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila (klatikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi wa taji hilo na kuwaongoza warembo wengine 15 waliokuwa wakiwania taji hilo. Wengine mshindi wa pili Camila Cindy John (kulia) na mshindi wa tatu Queenlatifa Hasim. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo.
Warembo wakipita jukwaani na kivazi cha ufukweni


 Vazi la ubunifu.

 Hii ndio tano bora kutoka kulia ni Miss Photogenic 2014, Getruda Massawe, Qeenlatifa Hasim, Maria Shila, Doreen Bene na Camila Cindy John.
 Jaji Mkuu wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania akitangaza tano bora.
 Warembo wakiwa jukwaani kabla ya kutangazwa 5 bora ya shindano hilo 2014

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog