KAGERA SUGAR: TUMEGONGA MWAMBA KUPATA MBADALA WA THEM FELIX `MNYAMA`, LAKINI TUMENASA VIJANA CHIPUKIZI Kitaifa
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAKATA miwa wa Kaitaba, Kagera
Sugar, rasmi wameanza kambi kujiwinda na mikikimikiki ya ligi kuu soka
Tanzania bara inayotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange amezugumza na Mtandao huu na kufafanua kuwa jana walifika Bukoba kambini na leo hii ndio wameanza kusaka kasi mpya kuelekea msimu mpya.
“Mungu ametusaidia tumefika Bukoba kambini jana, kwahiyo leo tumeanza kambi yetu rasmi kujiwinda na ligi kuu”. Alisema Kabange.
Kabange aliongeza kuwa kusogezwa
mbele kwa michuano ya ligi kuu ni faraja kwao kwani watapata muda mzuri
wa kukijenga kikosi chao kilichosheheni vijana wapya.
“Ni kweli ligi imesogezwa mpaka septemba 20, kwa upande mwingine ni nafuu kwetu ili tuweze kujipangga vizuri”.
“kama unavyojua, tuna vijana
wengi wapya, kwahiyo naona kwetu inakuwa faraja, tutaweza kuwaweka
pamoja wachezaji wapya na wa zamani. Tunashukuru kwa kuweza kupata muda
huu ulioongezwa”. Aliongeza Kabange.
Kuhusu matatizo ya kikosi chao
msimu uliopita ambao walishika nafasi ya tano kwa kujikusanyia pointi
38, Kabange alisema: “Sisi tulikuwa na usumbufu zaidi katika safu ya
ushambuliaji, kama ulivyo wimbo wa Taifa Tanzania, tumejitahidi kadri ya
uwezo wetu kuchukua vijana chipukizi ambao wanaweza kutusaidia kama
tulivyowatengeneza”.
“Them Felix `Mnyama` ameondoka
kuelekea Mbeya City fc, tulikuwa na mpango na kocha wangu kuchukua
mshambuliaji kutoka Uganda, lakini mipango hiyo imeshindikana. Kwahiyo
wachezaji tuliowasajili ni Watanzania watupu na naamini tukifanya nao
mazoezi tunaweza kufika pale tulipokusudia”. Alifafanua Kabange

mazoezi tunaweza kufika pale tulipokusudia”. Alifafanua Kabange.
0 maoni:
Post a Comment