Bado
mabishano ya kuwalinganisha yataendelea bila kujali nini kitatokea
kesho jumapili, vinginevyo Messi anamaliza maisha yake ya soka kwa
kutwaa kombe la dunia, hapo sasa atawashawishi wengi kuwa mkali kama
Maradano na Pele.
WAKATI
umewadia. Mara nyingi kumekuwepo na mjadala wa nani mkali kati ya Diego
Maradona na Lionel Messi. Wengi wanasema Messi hajashinda kombe la
dunia, lakini jumapili ya kesho nahodha huyo wa Argentina anaweza
kumaliza kila kitu.
Nyota
huyo mwenye miaka 27 itasimama kwa dakika 90 tu zitakazoweza kumfanya
kuwa mchezaji mkubwa zaidi duniania ambaye ameweka kila aina ya rekodi,
makombe, magoli na vinginevyo.
Mfungaji huyo wa muda wote wa Barcelona
akiwa na mabao 354, Messi ameshinda makombe 21 akiwa na wakatalunya, ni
mchezaji pekee katika historia kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia
(Ballons d`Or) mara nne mfululizo na pia aliongeza medali ya dhahabu ya
Olympic na kombe la dunia la vijana chini ya miaka 20 akiwa na jezi za
taifa lake. Kuna kitu kimoja tu kinakosekana.
Kama
alama ya taifa, Maradano aliiongoza Argentina mwaka 1986, naye Messi
anacheza fainali yake ya kwanza ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani.
Bado
watu wanabishana kuwalinganisha wakali hao kwa kuangalia utaifa wao,
staili moja ya uchezaji na magoli mengi waliyofunga, lakini kiukweli,
Messi amepata mafanikio makubwa zaidi ya kocha huyo wa zamani wa
Argentina kwa ngazi ya klabu hasa unapoangalia magoli na makombe.
0 maoni:
Post a Comment