Saturday, July 12, 2014


Maafisa wa usalama nchini Brazil

Afisa mmoja mwandamizi nchini Brazil Jose Mariano Beltrame amesema kuwa mji wa Rio de Jeneiro unajiandaa kuweka usalama wa hali ya juu katika historia ya fainali ya kombe la dunia kati ya Argentina na Ujerumani siku ya jumapili.
Zaidi ya maafisa elfu ishirini na tano wa polisi,maafisa wa zima moto,pamoja na majeshi yatashirikishwa katika hatua hiyo.
Rais wa Brazil Dilma Roussef anatarajiwa kuhudhuria fainali hizo katika uwanja wa Maracana akiandamana na marais wengine tisa akiwemo rais Vladmir Putin wa Urusi na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.
Meli ishirini na tano zitakuwa zinapiga doria katika pwani ya mji huo.
Usalama vilevile utaimarishwa katika maeneo ambayo maelfu ya raia wa Argentina wanapiga kambi.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog