Saturday, July 12, 2014


Liverpool imethibitisha kwamba wamekubali kumuuza Straika wao Luis Suarez kwa Barcelona.
Wiki ijayo Suarez atasafiri kwenda Barcelona kupimwa Afya yake na kusaini Mkataba wa Miaka Mitano.
Hivi sasa Suarez yupo kwenye Kifungo cha Miezi Minne alichopewa na FIFA baada kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy huko Brazil hapo Juni 26.

Tanga mwanzoni mwa Msimu uliopita Suarez amekuwa akitaka kuihama Liverpool na Mwaka Jana bado kidogo ahamie Arsenal ambao walitoa Ofa ya Pauni Milioni 40 na Pauni Moja juu ili kumnunua lakini walikataliwa.
Baada ya hapo Suarez akasaini Mkataba mpya wa muda mrefu na Liverpool na kuifungia Bao 30 kwenye Ligi Kuu England na kuibuka Mchezaji Bora wa Mwaka baada kuteuliwa na PFA, Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa huko England, na FWA, Chama cha Wanahabari wa Soka, pia cha England.
Inaaminika Barcelona wameafiki kulipa Dau la Pauni Milioni 75 ambalo ndio lipo kwenye Kipengele cha Mkataba wa Suarez na Liverpool ikiwa atataka kuhama kabla Mkataba wake kumalizika.
Ikithibitisha kuhama kwa Suarez, taarifa ya Liverpool ilisema: “Liverpool FC inathibitisha Luis Suarez ataondoka Klabuni baada kufikia makubaliano ya Uhamisho na FC Barcelona. Mchezaji sasa yupo huru kukamilisha taratibu za Uhamisho.”

If the shirt fits: Barcelona staff have already got on the job of printing Suarez's No 9 shirtsKwa upande wake, Suarez alitoa shukrani kwa Klabu na Mashabiki wake ambao amewataka kuelewa uamuzi wake. 

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog