Tuesday, June 16, 2015


Kenya 


Bingwa mtetezi wa voliboli ya wanawake barani Afrika,Kenya, Wameishinda Algeria kwenye mechi yake ya pili huku Senegal wakizidi kuwika katika mashindano ya voliboli ya kombe la mataifa ya Afrika yanayoendelea jijini Nairobi Kenya.
Nahodha wa Kenya Praxidis Agala alicheza kufa na kupona na kuongoza Kenya kuibwaga Algeria kwa seti 3-0 katika mashindano ya voliboli ya wanawake ya kuwania ubingwa wa mataifa ya Afrika.
Agala alionana vyema na seta Jane Wacu na kunyamazisha Algeria 25-20 seti ya kwanza, na ya pili Kenya ikashinda 25-22.
Kenya ilikamilisha kivuno hicho cha alama kwa kuichabanga alama 25-19 .
Huu ni ushindi wa pili kwa Kenya baada ya kuicharaza Mauritius seti 3-0 katika mechi yao ya kwanza Ijumaa.
Kenya inawania kushinda taji hili mara ya nane na kujikatia tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia itakayoandaliwa baadaye mwaka huu nchini Japan.
 null
Mshindi wa mashindano haya ataiwakilisha Afrika katika kombe la dunia litakaloandaliwa huko Japan
Senegal nayo inazidi kuwika kinyume na matarajio ya wengi.
Katika mechi ya kwanza Senegal ilishinda Cameroon seti 3-1 na leo hii ikanyamazisha Tunisia seti 3-2.
Katika matokeo mengine, Botswana ilishinda Mauritius seti 3-1 na Cameroon ikaizaba Morocco seti 3-0.
Jumatatu, Tunisia inapambana na Cameroon, Kenya dhidi ya Botswana, Morocco inamenyana na Senegal na Algeria dhidi ya Mauritius.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog