Tuesday, June 16, 2015


Timu ya taifa ya soka ya Uganda yenye wachezaji wanaocheza soka nyumbani imeanza maandalizi ya michuano ya mzunguko wa kwanza kufuzu kwa michuano ya Afrika CHAN itakayofanyika mwakani nchini Rwanda.
Uganda inajiandaa kuchuana na Tanzania siku ya Jumamosi mchuano utakaochezwa katika visiwa vya Zanzibar.
Kocha Milutin ‘Micho’ Sredojevic anasema baada ya mchuano wa mwishoni mwa juma lililopita wa kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017, kazi kubwa iliyo mbele yao ni kuikabili Tanzania.
Siku ya Jumanne, kikosi cha Micho kinaendelea na maandalizi yake katika taasisi ya mafunzo ya kiufundi ya Njeru ili kupata uzoefu katika uwanja wa bandia.
Kikosi kamili:
Makipa: Alitho James, Ochan Benjamin, Bwete Brian
Mabeki: Okoth Denis, Ntambi Julius ,Ochwo Brian, Musisi Farouk, Waswa Hassan, Bakaki Shafiq, Kiyemba Ibrahim, Okello Silvester
Viungo wa Kati: Bukenya Deus, Tekkwo Derrick, Mugerwa Yasser, Kizito Keziron, Mutyaba Muzamil, Eturude Abel, Kyeyune Saidi, Miya Farouk, Kiiza Martin
Washambuliaji: Sekisambu Erisa, Semazi John, Kalanda Frank, Ssentongo Robert, Fahad Muhamed Hassan

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, limempa kocha wa Stars Mart Nooij raia wa Uholanzi nafasi ya mwisho ya kuhakikisha kuwa kikosi chake kinafuzu katika michuano hii, la sivyo ajiuzulu.
Uamuzi huu ulitolewa na uongozi wa soka nchini humo baada kumalizika kwa michuano ya Kusini mwa mataifa ya Afrika COSAFA mwezi mmoja uliopita walikofungwa michuano yao yote.
Tanzania iliwahi kucheza katika michuano hii ya CHAN mwaka 2009 wakati makala ya kwanza ya michuano hii ilipofanyika nchini Cote Dvoire.
Kikosi cha Tanzania:
Salum Swedi, Kelvin Yondani, Amir Maftah, Juma Jabu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Shadrack Nsajigwa na Erasto Nyoni, huku viungo ni Nizar Khalfan, Shaaban Nditi, Mwinyi Kazimoto, Godfrey Bonny, Athuman Idd ‘Chuji’, Nurdin Bakary na Henry Joseph. Safu ya ushambuliaji ilikuwa chini ya Abdi Kassim ‘Babi’, Haruna Moshi ‘Boban’, Kigi Makassy, Mrisho Ngassa, Jerson Tegete, Mussa Hassan Mgosi.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog