Tuesday, June 16, 2015

AC Milan wamemteua Kocha wa zamani wa Serbia Sinisa Mihajlovic baada kumtimua Filippo Inzaghi.
Mihajlovic, ambae ni Beki wa zamani mwenye Miaka 46, amesaini Mkataba wa Miaka Miwili na kibarua chake cha mwisho kama Kocha kilikuwa huko Sampdoria ambako aliondoka mwanzoni mwa Mwezi huu.
Flippo Inzaghi, mwenye Miaka 41, alikuwa Mchezaji wa zamani wa AC Milan aliyoichezea kuanzia 2001 hadi alipostaafu 2012.
Inzaghi aliteuliwa kuwa Kocha wa AC Milan Mwezi Juni Mwaka Jana kuchukua nafasi ya Mchezaji mwenzake wa zamani Klabuni hapo Clarence Seedorf.
Lakini AC Milan, chini ya Inzaghi, haikufanya vyema na ilimaliza Nafasi ya 10 kwenye Ligi Serie A ikiwa Pointi 35 nyuma ya Mabingwa Juventus.
Akiwa Mchezaji, Mihajlovic alizichezea AS Roma, Sampdoria, Lazio na Inter Milan katika kipindi cha Miaka 20 ya maisha yake ya uchezaji na pia kuichezea Timu ya Taifa ya Nchini kwao Mechi 63.
Baada kustaafu kama Mchezaji akiwa na Inter Milan, Mihajlovic alianza kama Kocha hapo hapo akiwa Msaidizi wa Roberto Mancini na kisha kuziongoza Klabu za Bologna, Catania na Fiorentina na Aprili 2012 kuteuliwa kuwa Kocha wa Serbia.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog