Tuesday, December 9, 2014



Idris akishangilia kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi wa BBA Hotshots
Kijana mtanashati kutoka Tanzania, Idris Sultan amefanikiwa kuipeperusha vyema bendera ya nchi yake kwa kutawazwa kuwa mshindi wa shindano la Big Brother Hotshots lililofikia tamati yake usiku wa jana(Nov 7) nchini Afrika kusini baada ya kukaa mjengoni kwa takribani siku 63 ambazo ni sawa na miezi miwili pasipo kutoka nje.
Idris alifanikiwa kumgaragaza mpinzani wake raia wa Nigeria, Tayo aliyeingia nae katika fainali ya shindano hilo kwa kupigiwa kura nyingi zaidi na mashabiki wake zilizomuwezesha kunyakua kiasi cha dola za marekani 300,000 ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa mshindi wa kwanza kama ilivyotangazwa hapo awali.
Mashabiki, wadau na watu mashuhuri kupitia mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na Instagram wamempongeza Idris kwa ushindi sambamba na kuliwakilisha ipasavyo Taifa la Tanzania.
Tazama hapo chini picha zaidi za matukio yaliyojiri hapo jana ndani ya mjengo wa BBA

Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20142
Idris akiwa shangilia kwa hisia kali ushindi wake
Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-2014006
Idris wa pili kushoto akipongezwa na washiriki wenzake kwa kuibuka mshindi
Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-2014007
Idris akihojiwa mara baada ya kutawazwa kuwa mshindi
Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-2014009
Idris akishika kioo kinachoonyesha dola laki 300,000 za kimarekani alizoshinda
Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140010  Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140013 Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140022 Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140032 Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140042

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog