Saturday, June 13, 2015



Winga Memphis Depay amekamilisha Uhamishi wake wa Pauni Milioni 31 kujiunga na Manchester United kutoka PSV Eindhoven ya Holland.
Depay, mwenye Miaka 21, amesaini Mkataba wa Miaka Minne ukiwa na nyongeza ya Mwaka Mmoja.
Wakiongea baada ya kusaini Mkataba, Depay alisema hii ni ndoto yake iliyotimia wakati Meneja wa Man United, Louis van Gaal, alisema Mchezaji huyo ana nafasi kubwa kuwa mmoja wa Wachezaji bora kwenye Klabu hiyo.
Mwezi uliopita, Depay alifuzu upimwaji afya yake na kusubiri kusainiwa Mkataba.
Katika Msimu ulioisha Mwezi Mei, Depay ndie aliibuka akiwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Holland, Eredivisie, alipofunga bao 22 na kuibeba PSV Eindhoven kubeba Ubingwa wao wa kwanza wa Holland tangu 2008.

Memphis Depay akiwa na Meneja Van Gaal

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog