Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (kushoto),
akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria
Mganilwa ofisini kwake kabla ya kupokea magari mawili ambayo
yamekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Transaid la nchini Uingereza,
hafla ya kukabidhi magari hayo imefanyika leo asubuhi katika viwanja
vya NIT.
Taswira ya tanker trailer la futi 40 na Folk Lift
ambayo yamekabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) na
Kampuni ya Transaid leo asubuhi katika viwanja vya chuo hicho. Magari
hayo yatasaidia wanafunzi wanaosoma kozi za udereva chuoni hapo.
Sehemu
ya Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakimsikiliza
Mgeni Rasmi (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari
mawili kwa ajili ya kufundishia mafunzo ya udereva chuoni hapo, magari
hayo yalimekabidhiwa leo asubuhi na Shirika la Transaid la nchini
Uingereza.
Mkurugenzi wa Mradi ya Usalama Barabarani wa Shirika la Transaid la
Nchini Uingereza, Mr. Neil Rettie (mwenye tai ya blue) akimkabidhi
funguo za gari aina ya Iveco kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt
Shaaban Mwinjaka kwa ajili ya mafunzo ya Udereva yanayotolewa na Chuo
Cha Taifa Cha Usafirhsaji (NIT), Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja
vya chuo hicho leo Asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasha gari ya kuinulia mizigo focal lift
kama ishara ya kupokea moja ya magari mawili yaliyokabidhiwa na Shirika
la Transaid la nchini Uingereza kwa Chuo cha Taifa cha Usafirshaji
(NIT), leo asubuhi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka, akiwasha gari aina ya Folk Lift
lililokabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usarifshaji (NIT), kwa ajili ya
wanafunzi wataochukua mafunzo ya udereva chuoni hapo. Magari hayo
yamekabidhiwa leo asubuhi katika viwanja vya Chuo hicho.
0 maoni:
Post a Comment