Monday, March 10, 2014

    Arsenal na Bayern Munich nanone



     


    Pichani ni baadhi ya wachezi wa Arsenal na Bayern Munich.
    Michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya kuendelea leo usiku huku kukiwa na mechi mbili.
    Arsenal, inaelekea, Bonn, kutoana jasho na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munichambayo ilishinda mechi ya raundi ya kwanza kwa mabao mawili kwa nunge katika uga wa Emirates.
    Hata hivyo Arsenal itakosa huduma za mcheza kiungo wake Kieran Gibbs ambaye kwa sasa anauguza jeraha la mkuu na mshambulizi Yaya Sanogo, lakini mlinda lango Laurent Koscielny, ambaye alikuwa akiuguza jeraha la pajaanatarajiwa kurejea.

    Kipa Lukasz Fabianski naye atachukuwa mahala pa Wojciech Szczesny, ambaye amesimamishwa kucheza kwa muda baada ya kupewa kadi nyekundu wakati wa mechi ya raundi ya kwanza.
    Mwaka uliopita Arsenal iliishinda Bayern kwa magoli mawili kwa bila katika mechi ya marudiano lakini ilibanduliwa nje ya mashindano hayo baada ya kupoteza raundi ya kwanza 3-1.
    Katika mechi nyingine ya marudiano leo usiku itakuwa kati ya Atletico Madrid na AC Milan. Madrid ilishinda awamu ya kwanza kwa bao moja kwa bila.
    Mario Balotelli huenda akajumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji kumi na mmoja wa AC Millan, baada ya kuuguza jeraha la mgongo alilopata siku ya Jumamosi dhidi ya klabu ya Unidese.
    Atletico nayo inamkaribisha mchezaji wake aliyefunga idadi kubwa yua magoli Diego Costa huku ikijaribu kufunzu kwa robo fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka kumi na saba iliyopita.
    Na ili kufuzu, mabingwa hao mara saba wa Ulaya ni sharti waandikishe historia ya kuwa timu ya tatu katika historia ya kombe hilo kuwahi kushindwa nyubani katika mechi ya raundi ya kwanza na ishinde mechi ya marudiano ugenini.

    0 maoni:

    Post a Comment

    waliotembelea blog