Wakazi wa mtaa wa migombani kata ya segerea wakiwahoji matapeli ambao walikua wakijaribu kumfanyia utapeli dada mmoja
na hatimaye kushindwa kutimiza lengo lao mara baada ya dada huyo
kushtukia mbinu zao na kuomba msaada kwa wananchi na ndipo hapo
walipotiwa nguvuni na kupelekwa katika ofisi za serikali ya mtaa wa
migombani
Matapeli
(mwenye shati la draft) wakipewa kichapo mara baada ya kushindwa kujibu
maswali ya wananchi waliowakamata leo katika kituo cha daladala cha
Segerea
Mmoja
wa watumishi wa serikali ya Mtaa wa Migombani Kata ya segerea Mfaume
(wa kwanza kushoto Mwenye fulana ya njano) akijaribu kuwakata wananchi
hao kujichukulia sheria Mikononi mara baada ya kuwatia nguvuni matapeli
hao leo katika kituo cha daladala cha Tabata Segerea
Mmoja
wa matapeli akijizuia kichwani mara baada ya wananchi wenye hasira kali
wakiendelea kushusha kipigo kitakatifu, katika tukio la kujaribu
utapeli lililotokea muda mfupi katika kituo cha daladala cha segerea
mwisho
Hapa
tapeli wa pili (aliyeinamishwa kichwa) akiendelea kupokea maumivu
kutoka kwa wakazi wa segerea mara baada ya kukamatwa wakati wakitaka
kujaribu kutapeli
kipigo kikiendelea kutolewa kwa matapeli hao
Matapeli
wakiwa ndani ya ofisi ya serikali ya mtaa wa migombani mara baada ya
kupokea kipigo cha mbwa mwizi muda mfupi uliopita katika kituo cha
daladala cha segerea mwisho wakati wakijaribu kutapeli
Baadhi
ya wakazi wa mtaa wa migombani kata ya segerea wakichungulia dirishani
katika ofisi za serikali ya mtaa wa migombani kwaajili ya kushuhudia
matapeli waliopokea kichapo cha mbwa mwizi mara baada ya mbinu zao kufua
dafu na kushtukiwa
0 maoni:
Post a Comment