Weekend
iliyopita msanii wa muda mrefu wa muziki wa Dancehall Hard Mad ametoa
wimbo mpya ambao ni jibu la hit song ya Lady JayDee ‘Yahaya’. Swali la
Jide “Yahaya unaishi wapi” ndio limezaa jina la wimbo wa Hard Mad aliyejibu ‘Naishi Ghetto’, na mambo mengine yote yaliyoimbwa katika wimbo huo ni majibu ya maswali ya ‘Yahaya’.
Hard
Mad amezungumzia jinsi wazo la kufanya wimbo wenye majibu ya ‘Yahaya’
lilivyopatikana, na kudai kuwa alilipata baada ya kukutana na mtu
aitwaye Yahaya anayeishi Kinondoni kama ilivyotajwa katika wimbo wa
Jide.
“Idea ilikuja kama hivi, kuna mshikaji mmoja amekuja kutoka Dar es salaam ambaye yeye ni mwana sana katika upande wa filamu…yeye ndio alinipa hiyo idea bwana blaza eeh mimi naitwa Yahaya naishi Kinondoni , sasa naona kama hii ngoma imenilenga nini nikamwambia hamna labda katika art tu ya mtu na nini na nini sababu wale Yahaya wanaoishi Kinondoni bado ni wengi”. Hard Mad alizungumza jana kupitia Showtime NewChapter ya Radio Free Africa, Mwanza na Renatus Kiluvia aka Bizzo.
Hard Mad aliendelea kusimulia kuwa baada ya Yahaya kumfuata alimwambia wimbo wa Jide umemsababishia awe na wakati mgumu kutokana na jinsi watu wanavyomchukulia sasa wakidhani anayeimbwa ni yeye kutokana na mambo mengi yaliyoimbwa yanamhusu moja kwa moja.
“Akaniambia ndio lakini inaniuma sana lakini mimi nilikuwa naishi na watu vizuri naendesha mandinga ndinga za watu wananiamini lakini saizi naona kila mtu ninaemfuata ananiambia we Yahaya tu unajua zile.” Alisema.
“Alivyokuja ndio akaniambia bwana blaza mi sio msanii lakini hii idea unaweza kuifanyia kitu flani kwasababu wewe ni msanii wa zamani na sikuwaza kama nitakutana na wewe studio kama hivi nilikuwa nakusikia tu kwenye radio na kukuona kwenye TV nashukuru nimekuona labda unaweza ukanifanyia kitu kuhusiana na hili ili roho yangu na mimi isuuzike.”
Hard Mad ameendelea kusema kuwa baada ya kupewa idea na Yahaya aliusikiliza vizuri wimbo na kujaribu kuanza kutengeneza jibu,
“Kwahiyo ndio hivyo idea ilivyokuja na mimi nikakaa nikaisikiliza nikajaribu kufanya kitu naona na kitu kikakua na pia katika upande mmoja au mwingine nikawa nimeona kama ni art pia kwasababu hata ukisikiliza miziki ya zamani ya kina Marijani Rajab, Msondo ukisikiliza Juwata Jazz kuna design flani walikuwa wanafanya ya music, kwamba huyu anaweza akatoa swali mwingine akajibu na ndo kitu ambacho kilikuwa kinafanya hasa ukue katika kiwango kikubwa sana hapa nchini.
Lakini sikuhizi naona hicho kitu kinaenda kinakufa hata watu wakijibu wanakuwa yani hata kama mtu ameuliza swali wengine wanaogopa kujibu wanaona kama watabeef, lakini mi nahisi sio kubeef ni kwamba unafanya sanaa inakuwa na changamoto.” Alisema Hard Mad.
Msikilize Hard Mad hapa
Man Water kushoto
Ukiskiliza vizuri beat ya ‘Naishi Ghetto’ ni kama ile ile ya Yahaya lakini imepigwa upya, producer wa ‘Yahaya’ ya Anaconda, Man Water wa Combination Sounds pia amezungumzia wimbo huo na kudai kuwa yeye hajahusishwa kwa namna yoyote katika kuombwa idhini ya kutumiwa kwa ubunifu wa kazi yake katika wimbo wa Hard Mad.
“Maoni yangu na kwa jinsi nilivyoiskiliza kwanza kitu kimenishangaza isipokuwa huwa najua harakati za kuna vitu vinaitwa riddim, yaani mtu unaweza ukaendeleza idea au ukaonesha unashow love kwenye idea ambayo watu wameshaianzisha. Lakini hii naona iko tofauti kwasababu hakuna taarifa yoyote lakini kwasababu hata kama utapata go ahead kutoka kwa msanii bado unatakiwa upate Baraka zote kutoka kwa producer kwasabbau hata Jide mwenyewe Yahaya ni kwamba aliikuta beat si kwamba alikuja akaniimbia ili nitengeneze beat.” Alisema Water
“Mi naona kilichofanyika si sawa kwasababu hakukuwa na mawasiliano, unaweza ukapewa go ahead kwamba poa baada ya kusikiliza unataka kuimba nini lakini naweza nikakubali hayo yote sababu pengine ni namna ya mtu kutafuta namna ya kutoka, na wakati mwingine tukiwa tunazizungumzia mambo haya kama hivi ndio tunazidi kumpa mtu credit, lakini mi naona bigup apewe yule mtu ambaye alianzisha idea big up to Lady JayDee afu big up to Combination Sounds Kombinenga.” Aliongeza Man Maji wa Kombinenga
Water amesema kuwa nyimbo kama hizo huwa ni za kiharakati tu na hazistahili kuchezwa kwenye radio bali zinafaa kusambazwa katika mitandao ya kijamii peke zaidi.
Man Water aliulizwa juu ya hatua anazopanga kuchukua baada ya kuusikia wimbo huo wa Hard Mad:
“Haya mambo ya haki miliki bado vitu vingi havijakaa sawaswa watu wengi sana wanauchezea muziki wanachezea pia kazi za watu wengi sana. Kwahili siwezi kusema chochote ni mapema sana kwasababu track nimeisikia leo, sijazungumza na Jide kama kuna taarifa zozote lakini ninauhakika kwasababu track haijatendewa haki kama vile iko chini ya kiwango sisemi kwa ubaya lakini ukizi compare unaweza ukaona mmoja anaeleweka anaongea nini mwingine haeleweki.”
Water ameonesha kutokuwa na tatizo na Hard Mad kwasababu wanafahamiana vizuri, isipokuwa amesisitiza kitu ambacho hakubaliani nacho ni kitendo cha kutopewa taarifa mapema na wahusika.
“Lakini pia Hardmad ni mwanangu hata hivyo nimeshangaa kwasababu Hard Mad kwanini asizungumze na mimi afu ni mshikaji wangu sana tena sio kitoto kiasi kwamba hata akisikia mimi nazungumza nay eye kupitia media kama hivi anaweza na yeye akashtuka kidogo lakini ni mtu ambaye tuko naye Kino tunaweza tukazungumza….tukatoa Baraka za ile go ahead ya kufanya anachokifikiria kufanya, lakini sivyo hivi alivyofanya sababu yeye kama ni msanii mkubwa sijui analeta picha gani kwa wasanii ambao wanachipukia wanaweza wakaona hii ndio njia sahihi ya kutoa track.”
Msikilize Man Water
Hard Mad |

0 maoni:
Post a Comment