Tuesday, November 12, 2013


MSAADA
Nakukubali sana, napenda unipe nafasi niwe chini ya lebo yako. Geofrey, Kibaha, 0713434329
BOB JUNIOR: Njoo studio kwangu (Sharobaro) nikusikilize kama unafaa basi nitakuchukua tufanye kazi pamoja.

ANATOKA NA AUNT LULU?
Bob Junior nataka kujua, eti wewe unatoka kimapenzi na Aunt Lulu (Lulu Mathias), mlimbwende wa Kimwana Manywele? Salim Liundi, Dar, 0658110395
BOB JUNIOR: Hapana.


KWA NINI AMEACHANA NA MKEWE?
Bob Junior upo fresh kwenye gemu lakini mbona umemuacha mkeo na kuanza kumsifia Vanessa Mdee kwenye media? Unataka kumuoa? Mama Un, Dar, 0757715360
BOB JUNIOR: Mke wangu nimeachana naye kwa sababu za kifamilia, Vanessa ni mwanamke mzuri anapaswa kusifiwa.

KUUZA SURA
Kwa nini wasanii wengi wanaotolea nyimbo kwako unataka mpaka na wewe uuze sura kwenye video? Jakobo, Dar, 0689619817
BOB JUNIOR: Mara nyingi huwa naweka lebo yangu kutokana na wasanii wenyewe kutaka nifanye hivyo.

AMEZAA NJE YA NDOA?
Bob Junior uko vizuri sana hasa kwenye kuimba. Mtaani kuna tetesi kuwa una mtoto mwingine wa kike nje ya ndoa. Je, ni kweli? Raphael, Morogoro, 0713850820
BOB JUNIOR: Hapana mimi nina mtoto mmoja tu niliyempata ndani ya ndoa.

HUYU ANATAKA KUJUA

Bob Junior mtoto wako anaitwa nani na mnaishi wapi? Msomaji, 0682022412
BOB JUNIOR: Mtoto wangu anaitwa Rummy, ninaishi Magomeni-Mapipa, Dar.

YEYE NA WEMA VIPI?
Bob Junior uliwahi kutoka kimalavidavi na Wema na kumsababishia kipigo kutoka kwa Diamond (Nasibu Abdul). Erasto, Dar, 0765302086
BOB JUNIOR: Sina jibu.

BIFU NA DIAMOND
Nasikia wewe na Diamond mna bifu la chini kwa chini, ni kweli? Davy Ruta, Mwanza, 0769666622
BOB JUNIOR:

STAILI YA MUZIKI

Nakupa big up Bob Junior kwa kuwa mfano bora, vipi mipango yako ya baadaye hufikirii kubadili aina ya uimbaji wako ukaanza kuchana? Msomaji, 0719041057
BOB JUNIOR: Asante, sina mpango huo kwa sababu kuchana hakuna biashara.

NI KWELI DIAMOND ALIMPIGIA MAGOTI?

Bob Junior napenda sana staili yako ya uimbaji. Je, ni kweli Diamond alikuja kupiga magoti kwako? Fred Boy, Dar, 0656552592
BOB JUNIOR: Kweli alishaomba msamaha.

ANA MARINGO?
Nakupenda sana Bob Junior ila unachonikera ni maringo tu, jaribu kuwa kama JB (Steven Jacob) mbona utakuwa poa tu! Msomaji, 0655542810
BOB JUNIOR: Mimi sina maringo huo ni mtazamo wako tu.

MAUNO JUKWAANI

Kwa nini Bob Junior unapenda kukatika mauno jukwaani? Msomaji, 0753630184
BOB JUNIOR: Ninakata mauno kwa sababu muziki wangu unaruhusu.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog