Mwanamuziki
nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja joto
ya kiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa kila kitu
pamoja na gari yake.
Mwanamuziki
huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta
Jijini Dar pamoja masisita du wakila bata ghafra kundi la watu watano
lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na
kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao
wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.
Habari
zaidi toka kwa chanzo chetu kilichoshuhudia timbwiri hilo
kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa
mjini aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini na
huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa bongo
movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne msanii
huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo baada
ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya
Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo
chetu
Hata hivyo baada ya kumkamata
msanii huyo Evance alimpelekwa Oysterbay ambapo aliiacha gari na simu
kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo atapewa gari yake.
0 maoni:
Post a Comment