Sunday, August 16, 2015


Mame Diouf aliisawazishia Stoke Dakika za mwishoni na kupata Sare ya 2-2 walipocheza na Tottenham huko White Hart Lane kwenye Mechi ambayo Tottenham waliongoza 2-0.
Eric Dier ndie aliwapa Tottenham Bao la kwanza na Nacer Chadli kupiga la pili.

SUNDERLAND 1 vs 3 NORWICH
Norwich City wameichapa Sunderland kwao Stadium of Light Bao 3-1 na kupata ushindi wao wa kwanza Msimu huu.
Russell Martin ndie aliwapa Bao la kwanza baada ya Kipa Costel Pantilimon kulitema Shuti la Robbie Brady na Steven Whittaker kuwapigia Bao la Pili kufuatia pasi safi kati yake na Wes Hoolahan huku Bao la 3 likifungwa na Nathan Redmond.

Bao pekee la Sunderland lilifungwa na Kijana wa Miaka 21 Duncan Watmore kwenye Mechi yake ya kwanza kabisa kuichezea Timu yake.
Swansea wamewanyuka Mtu 10 Newcastle Bao 2-0 kwa Bao za Bafetimbi Gomis na Andre Ayew.
Newcastle walicheza Mtu 10 kuanzia muda mfupi kabla Haftaimu kufuatia Kadi za Njano mbili kwa Beki wao Daryl Janmaat na kasha kupewa Kadi Nyekundu

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog