Sunday, August 16, 2015


Manchester United wamemsaini Kinda wa Holland Timothy Fosu-Mensah na kumpa Mkataba wake wa kwanza kama Mchezaji wa Kulipwa, yaani Profeshenali.
Man United imetangaza habari hii kwenye Mtandao wao wa Twitter walipoposti Picha ya Fosu-Mensah akiwa na Meneja Msaidizi Ryan Giggs.
Fosu-Mensah huweza kucheza Kiungo na alitua Man United Mwaka Jana kutoka Ajax.
Inasemekana Meneja Louis van Gaal anamhusudu sana Kijana huyo ambae ndie Kepteni wa Timu ya Taifa ya Holland ya Vijana wa chini ya Miaka 17, U-17.
Kijana huyo sasa ataichezea Timu ya Vijana ya Man United ya U-21 chini ya Kocha Paul McGuinnes.

Manchester United wamemsaini Kinda wa Holland MANCHESTER UNITED WAPYA
Memphis Depay (PSV Eindhoven) Ada Haikutajwa
Matteo Darmian (Torino) Ada Haikutajwa
Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich) Ada Haikutajwa
Morgan Schneiderlin (Southampton) Ada Haikutajwa
Sergio Romero (Sampdoria) Ada Haikutajwa

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog