Sunday, August 16, 2015


image3Ninayo Good News imenifikia mtu wangu ambayo Watanzania wengi na wakazi wa Dar es salaam tulikua tukiisubiri kwa muda mrefu ni kuhusu kukamilika kwa mradi wa Mabasi yaendayo haraka ambayo zaidi ya mwaka na nusu yaliingia kwenye headlines za kuwa yatatoa huduma hizo.
IMG_0146Habari ikufikie kuwa Mabasi hayo rasmi yanaanza kazi August 17 Jumatatu kuanzia  saa 3 asubuhi nje ya kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo ambako kutafanyika uzinduzi wa kuanza huduma ya mpito kisha Wananchi wataruhusiwa kupanda mabasi hayo kutoka Ubungo kwenda Kimara na kutoka Kimara hadi Kivukoni Bure.
Kwa bara la Afrika,jiji la Dar es salaam litakua la pili kutekeleza mradi huu mtu wangu baada ya Afrika Kusini na litakua jiji la kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki,Kaskazini na Kati.
DeusiDedith Mutasingwa ambaye ni Afisa wa masuala ya fidia katika mradi wa mabasi haya yaendayo haraka yaliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za mitaa,amesema yapo mabasi ya aina mbili kuna yale ya mita 18 ambayo yana uwezo wa kubeba abiria 140 na yapo yenye uwezo wa kubeba watu 80.
image1Amesema mabasi hayo pia yamezingatia watu wenye mahitaji maalum kama Walemavu na Wajawazito,pia Wafanyabiashara wanaopanga vitu vyao pembeni ya Barabara na kwenye vituo wameombwa kuviondoa na kwa wale watakaonekana kukaidi amri hiyo faini yake si chini 250,000.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog